Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amezindua ndege mpya mbili za shirika za ATCL aina ya Bombardier Dash 8 Q400 katika uwanaja wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Akizindua ndege hizo rais Magufuli amewajibu wanaozibeza kuwa ni ndogo na hazina uwezo kwa kusema hizo ndizo ndege stahiki kwa hali ya viwanja vilivyopo na kipato cha watanzania.
Rais Magufuli pia amesema serikali ipo katika mchakato wa kununua mbili ndege mpya zitakazokuwa na uwezo wa kubeba watu zaidi ya 240 na nyingine 160 ambazo zitatumika kwa safari za nje ya Tanzania.
"Kwa sababu fedha za kununulia ndege hizo zote mbili kubwa zipo, tukinunua ndege ya kubeba watu 240 itakuwa inatoka hapa Dar es Salaam hadi Marekani bila kutua popote, itaondoka hapa Dar es Salaam mpaka China bila kutua popote ili watalii wanaotoka China, Marekani, Urusi, Ujerumani na nchi nyingine wasifikie nchi nyingine, watue hapa moja kwa moja na waangalie maliasili zetu tulizonazo, utalii wetu upande, na huo ndio mwelekeo wa nchi yetu tunaoutaka" amesema Rais Magufuli.
Shirika la ATCL litakuwa na safari za Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Tabora, na Musoma,pia upande wa kaskazini mashariki litakuwa na safari za Kilimanjaro, na Arusha, huku kusini litakuwa na safari za Mbeya na Mtwara.
No comments:
Post a Comment