UKUTA KUMEKUCHA-VIONGOZI WA CHADEMA WALIANZISHA RASMI - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Monday, August 22, 2016

UKUTA KUMEKUCHA-VIONGOZI WA CHADEMA WALIANZISHA RASMI

 


Viongozi wa CHADEMA wameanza rasmi kutawanyika mikoani kwa ajili ya operesheni ya UKUTA.

Mwenyekiti Freeman Mbowe ameripotiwa kuwepo kanda ya kaskazini, huku aliyekuwa mgombea wa urais katika uchaguzi uliopita kupitia tiketi ya chama hicho Edward Lowassa akiwa ameshawasili mkoani Mbeya na anatarajiwa kuanza mara moja mikakati ya vikao kwa ajili ya zoezi hilo.

Mbowe jana amekutana na viongozi wa kanda ya kaskazini na kuunda kamati zitakazofika katika majimbo yote 35 ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.


Hata hivyo Mbowe amesisitiza kuwa bado mlango wa mazungumzo na serikali kwa ajili ya kusitisha oparesheni hiyo upo wazi na kama serikali itaaamua kukaa nao meza moja watakuwa tayari kusitisha zoezi hilo.

Zoezi la oparesheni UKUTA limeandaliwa na umoja wa katiba ya wananchi(UKAWA) na kupata upinzani mkali kutoka serikalini ikiongozwa na vyombo vya usalama, na hali ya usalama imehofiwa kutokana na hofu ya kutokea machafuko nchini kutokana na msuguano wa pande hizo.


No comments: