Mwanamke mmoja ameuawa na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa nchini Thailand baada ya mabomu mawili kulipuka katika mgahawa maarufu wa Hua Hin unaopendelewa na Mfalme Bhumibol Adulyaj.
Mwanamke aliyeuwawa ni raia kutoka Thailand lakini kwa upande wa majeruhi wanahisiwa kuwa raia wa kigeni.
Mkuu wa polisi Samer Yousamran, amesema majeruhi wanatibiwa hospitalini.
Kwa mujibu wa Polisi, mabomu hayo yalikuwa yamefichwa kwenye sufuria na kulipuliwa na simu.
Hadi sasa haijajulikana ipi haswa nia ya waliohusika kulipua mabomu hayo.
No comments:
Post a Comment