MAREKANI, IRAN NA SYRIA ZATUNISHIANA MISULI.Marekani yapeleka ndege za kivita - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Sunday, August 21, 2016

MAREKANI, IRAN NA SYRIA ZATUNISHIANA MISULI.Marekani yapeleka ndege za kivita

Ndege ya jeshi la Marekani nchini SyriaNdege za jeshi la Marekani zimepelekwa mji wa Hassakeh nchini Syria kuwalinda wanajeshi maalum wa Marekani walio mjini humo kutoka kwa mashambulizi ya angani ya Syria.
Makao makuu ya jeshi la Marekani yanasema kuwa ndege za Syria zilikuwa zikiondoka wakati ndege za Marekani zilipowasili.
Watu katika mji wa Kaskazini Masharikia wa Syria wanasema kuwa ndege za serikali zilishambuliwa mitaa yenye wakurdi kwa muda wa siku mbili zilizopita ambapo maelfu ya watu wanaripotiwa kuyakimbia makwao.
Serikali ya Syria imekuwa ikisaidiwa kwa karibu na Iran hiuku wanamgambo wa YPG wakisaidiwa na Marekani hivyo choko choko hizo kwa wanajeshi wa Marekani zimeonekana kama kutunishiana misuli kati ya nchi hizo.

No comments: