WAANDAMANAJI KENYA WATUMIA DAMU YA NG'OMBE KUPINGA WABUNGE KUJIONGEZEA MISHAHARA - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Tuesday, June 11, 2013

WAANDAMANAJI KENYA WATUMIA DAMU YA NG'OMBE KUPINGA WABUNGE KUJIONGEZEA MISHAHARA


http://www.kiswahili.rfi.fr/sites/kiswahili.filesrfi/imagecache/rfi_43_large/sites/images.rfi.fr/files/aef_image/Kenyan%20mps%20demand%20high%20slary.jpg 
NAIROBI-KENYA,
Mamia ya waandamanaji jijini Nairobi nchini Kenya kwa mara nyingine wamevamia majengo ya bunge kupinga mpango wa wabunge nchini humo kujiongezea mshahara.
Wakiongozwa na wanaharakati wa haki za binadamu waandamanaji hao wamesema wamechoshwa na tabia ya wabunge hao kujiongezea mshahara mara kwa mara na kukataa mapendezo ya tume inayoshughulikia mishahara ya watumishi wa Umma iliyopunguza mshahara wao.
Kwa miezi kadhaa sasa, waandamanaji hao wamekuwa wakipinga hatua ya wabunge kutaka kulipwa Shilingi Laki nane za Kenya badala ya Shilingi Laki tano zilizopendekezwa na tume hiyo.
Waandamanaji hao wametumia damu ya ng'ombe na sanamu ya nguruwe kuonesha ulafi wa wabunge hao pamoja na pesa bandia wanayoita “Pesa Pig” kuwapa wabunge hao wakiingia kwenye vikao vya bunge.
Tume ya kushughulikia mishahara ya watumishi wa umma inaungwa mkono na wanaharakti hao imejitetea na kusema kuwa iliamua kupunguza mishahara ya wabunge baada ya kubaini kuwa walikuwa wanalipwa mshahara mkubwa zaidi duniani na pia kutokana na sababu za kiuchumi.
Wabunge kwa upande wao wanasema hawawezi kukubali mshahara uliopendekezwa kwa kile wanachosema tume hiyo haikufuata utaratibu unaostahili kabla kufikia uamuzi huo na wametishia kuupunguza mshahara wa rais na Jaji Mkuu.
Mwezi uliopita, maandamano mengine yalifanyika nje ya majengo ya bunge wakitumai nguruwe kuonesha gadhabu zao.
Rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri Raila Odinga kwa upande wao wamewataka wabunge hao kuacha harakati zao za kutaka kulipwa mshahara mkubwa na badala yake kuwafanyia kazi wakenya.CHANZO:RFI)

No comments: