TAIFA STARS YALALA 2-1KWA MOROCCO. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Sunday, June 9, 2013

TAIFA STARS YALALA 2-1KWA MOROCCO.


Matumaini ya Tanzania kushiriki michuano ya kombe la dunia yameanza kupotea baada ya leo hii kufungwa na Morocco kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kugombania nafasi ya kwenda Brazil 2014.

Mchezo huo uliofanyika Morocco, Stars walimaliza mechi wakiwa pungufu baada ya Aggrey Morris kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza baada ya kumchezea madhambi Abderazak Hemed hivyo kupelekea Morocco kupata penati iliyowapa bao la kuongoza.

Kipindi cha pili Morocco wakaongeza bao la pili dakika ya 50 kupitia Youssef El Arabi kabla ya Amri Kiemba kufunga bao la Stars dakika 10 baadae. 

Kutokana na matokeo haya Stars wanabaki nafasi ya pili kwa pointi 6 nyuma ya Ivory Coast wanaongoza kwa pointi 10 huku kumebakiwa na michezo miwili miwili katika kundi A linalojumuisha pia timu ya Gambia.

Stars wamebakiwa na mechi dhidi ya Ivory Coast itakayopigwa taifa na Gambia itakayopigwa ugenini.(CHANZO:SHAFIH DAUDA)

No comments: