MAREKANI,
Baada ya kampeni za miezi kadhaa , vituo vya kupiga kura
vimeshafunguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wenye ushindani mkali na
ambao ulikuwa na kampeni zenye kugharimu pesa nyingi zaidi kuwahi tumika katika
historia za uchaguzi Marekani.
Katika kampeni za mwisho Rais Obama alitoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa
kisiasa uliofanyika katika jimbo la Iowa hapo jana, ambapo kwa hisia alitokwa na machozi."Nimerudi tena nawaomba mtusaidie kumaliza tulichokianza, hapa ndipo mabadiliko yalipoanzia"Alisema Obama.
Ushindani katika uchaguzi huu ni mkali sana na mpinzani wa rais Obama wa
chama cha Republican Mitt Romney amekuwa akiyazulu mara kwa mara majimbo mawili
makuu Ohio na Pennsylvania.
Kura ya mwisho ya kutafuta maoni iliashiria kuwa rais Obama anaongoza katika
majimbo mengi ambayo wagombea wote wana nafasi.
Lakini kura hiyo inaashiria pia huenda idadi ya watu watakao jitokeza kupiga
kura ikawa kubwa miongoni mwa wafuasi wa Romney.
Kura za kwanza zilipigwa katika eneo la Dixville Notch katika jimbo la New
Hampshire ambapo wagombea wote walitoka sare.
No comments:
Post a Comment