MANCHESTER CITY WAIBWAGA MAN U!- Waifunga 1-0. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Tuesday, May 1, 2012

MANCHESTER CITY WAIBWAGA MAN U!- Waifunga 1-0.

Manchester, Uingereza, 

Manchester City wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuchukua tangu mwaka 1968 baada ya hapo jana kuifunga Manchester United kwa goli moja kwa bila kupitia nahodha wao Vincent Kompany katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad. Katika mchezo huo Manchester City ndiyo walikuwa timu bora katika kiwango huku wakitumia kikosi kile kile walichokitumia katika mchezo wao kabla ya huo dhidi ya Wolves tofauti na wapinzani wao Manchester United waliojaza viungo watano katikati ambapo Park Ji-Sung aliongezwa akisaidiana na wakongwe wengine Paul Scholes na Ryan Giggs.
Manchester United waliouanza mchezo kwa kasi walijikuta wakigeuziwa kibao katika robo ya mchezo huo na wenyeji kuanza kutawala huku Carlos Tevez alifanikiwa kuipenya ngome ya Manchester United katika dakika ya 16 na kutoa krosi ambayo hata hivyo iliondolewa na Phil Jones.

Hatimaye katika dakika ya 46 ya nyongeza ya kipindi cha Kwanza Vicent Kompany alifanikiwa kuunganisha vizuri kona iliyopigwa kutoka upande wa kushoto wa Man United  kwa kichwa na kuipa goli la kuongoza na la ushindi timu yake hiyo.

Hata hivyo baadae mchezo huo ulitawaliwa na misuguano ya hapa na pale ambapo katika kipindi cha pili kocha wa manchester City  Roberto Mancini na mwenzake wa Manchester United Alex Ferguson nusura wakunjane  baada ya Mancini kulalamikia kadi ya njano aliyopewa mchezaji wake Nigel De Jong  ambapo Ferguson alimshambulia Mancini na kumuonesha ishara kuwa yeye ni mlalamishi sana na walipokaribiana walizuiwa na kila mmoja kurudishwa upande wake, ingawa mwisho wa mchezo makocha hao walishikana mikono.

Licha ya kupambana kufa na kupona katika dakika za majeruhi Manchester United hawakuweza kubadilisha matokeo hayo.Kwa ushindi huo Manchester City inashikilia usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 83 baada ya michezo 36 sawa na wapinzani wao wa karibu Manchester United  wenye pointi 83 pia ingawa wanazidiwa magoli ya kufunga na kuizidi magoli ya kufungwa manchester City.

No comments: