BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI TANZANIA, NANI KUWEPO TENA? - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Monday, April 30, 2012

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI TANZANIA, NANI KUWEPO TENA?


DAR ES SALAAM
 Siku chache baada ya Kamati kuu ya chama cha mapinduzi ya CCM kukubaliana na mapendekezo ya uongozi wa wabunge wa chama hicho wa kuwataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali kujiengua katika nafasi zao hali imeonekana kuwa tete kwa mawaziri ambao hawana tuhuma ila watalazimika kusubiri uteuzi mpya baada ya baraza la mawaziri kuvunjwa, huku habari kutoka katika baadhi ya vyanzo zikibainisha kuwa baraza hilo litakuwa na sura mpya kwa asilimia kubwa.

Katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye  aliangaza mpango wa rais kusuka upya baraza la mawaziri hapo juzi  muda mfupi baada ya kikao cha kamati kuu ya CCM(CC) kumalizika.
Katika bunge lililopita ulizuka mjadala na mvutano mkubwa kuhusu hatua ya kushinikiza baadhi ya mawaziri kujiuzulu kutokana na kushindwa kuwajibika.

Mawaziri waliotakiwa kujiuzulu kutokana na kashfa tofauti ni Mustafa Mkulo (Fedha na Uchumi) Cyril Chami (Viwanda na Biashara) William Ngeleja (Nishati na Madini) na Omar Nundu (Uchukuzi).

Wengine ni Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), George Mkuchika (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Profesa Jumanne Maghembe (Kilimo Chakula na Ushirika) na Dk. Haji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii).

  Lakini inahofiwa pia rais akapunguza ukubwa wa baraza lake hilo ambalo kwa sasa lina jula ya mawaziri 51 na kuwa na idadi pungufu zaidi ya hapo.Hata hivyo bado baadhi ya wachunguzi wa mambo wameonekana kupeleka tuhuma kwa rais mwenyewe zaidi ya watendaji wake huku wangine wakidhani yeye ndiye mwenye kupasa kuwajibika baada ya kushindwa mara kadhaa kwa watendaji wake.

No comments: