YANGA MABINGWA ASILIMIA 99.5 - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Tuesday, May 16, 2017

YANGA MABINGWA ASILIMIA 99.5



Ushindi wa Yanga wa goli 1-0 dhidi ya Toto Africans unaifanya Yanga kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kufikisha pointi 68 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi tatu.

Goli pekee la Yanga katika mchezo wa leo limefungwa na Tambwe dk.81 kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Juma Abdul.

Ikiwa imebaki mechi moja kabla ya ligi kumalizika, Simba inahitaji kushinda mechi yao dhidi ya Mwadui FC kwa idadi kubwa ya magoli halafu Mbao nayo iifunge Yanga kwa idadi kubwa ya magoli ili Simba itwae taji la VPL kitu ambacho ni kigumu kulingana na hali ilivyo kwa sasa.

Katika mchezo wa leo haikua rahisi kwa Yanga kupata ushindi dhidi ya Toto kwa sababu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilikua hazijafungana. Goli pekee kwenye mchezo huo limefungwa na Amis Tambwe dakika ya 81 ya mchezo.

Ikiwa Yanga watalitwaa taji la ligi msimu huu itakua ni mara yao ya tatu mfululizo kulibeba taji hilo kuanzia msimu wa 2014-15, 2015-16 na msimu huu 2016-17.

Toto wanaendelea kubaki kwenye hatari ya kushuka daraja wakiwa nafasi ya 15 kwa pointi zao 29 wakiwa wamebakiza mechi moja dhidi ya Mtibwa Sugar.


CREDITS: SHAFIH DAUDA SPORTS.

No comments: