YANGA YAUA 6-2 KAGERA, AZAM YAFUTA MKOSI - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Sunday, October 23, 2016

YANGA YAUA 6-2 KAGERA, AZAM YAFUTA MKOSI

YANGA wameanza rasmi mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara – baada ya leo kuwatandika wenyeji Kagera Sugar mabao 6-2 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Ushindi huo wa kwanza mkubwa zaidi msimu huu, unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 21 baada ya kucheza mechi 10 na kupanda hadi nafasi ya pii, nyuma ya Simba SC yenye pointi 26. 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Suleiman Kinugani aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha na Nicholas Makalanga, hadi mapumziko Yanga walikuwa wanaongoza 3-1.

Kipindi cha pili, Kagera wakaanza vizuri na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 49, mfungaji yule yule Mbaraka Yussuf aliyetumia makosa ya mabeki wa Yanga.

Hata hivyo, Yanga wakaamsha hasira zao na kufanikiwa kupata bao la nne lililofungwa na Deus Kaseke dakika ya 58 kwa shuti akimalizia krosi ya Msuva.
Chirwa akaifungia Yanga bao la tano akimalizia mpira uliotemwa na kipa Burhan baada ya shuti la Ngoma.

Donald Ngoma akakamilisha ushindi mnono wa Yanga leo kwa kufunga bao la sita dakika ya 64 baada ya kuambaa na mpira na kumchambua Burhan kufuatia pasi ya Haruna Niyonzima.



Katika mchezo mwingine Azam FC ikiwa nyumbani imepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.

Matokeo ya mechi zote tarehe 22.10.2016:




No comments: