Ligi Kuu bara imeendelea tena leo kwa michezo mitano katika viwanja mbali mbali, ambapo mkoani Mwanza timu ya Young Africans imefanikiwa kuinyosha Toto Africans kwa magoli mawili yaliyofungwa na Obrey Chilwa dk.29 na Simon Msuva dk.55.
Katika michezo mingine Stand United imelala magoli 2-1 ugenini dhidi ya Prisons ya Mbeya, Mbeya City 1-1 Ndanda, Ruvu Shooting 1-1 Mwadui, Maji Maji 2-0 African Lion.
No comments:
Post a Comment