DROO ZA AFCON USIKU HUU - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Wednesday, October 19, 2016

DROO ZA AFCON USIKU HUU

Droo ya Afcon inafanyika usiku huu huku katika mji wa De' L'Amitie mjini Gabon
Washiriki wote 16 na mamilioni ya watu kote duniani wana shauku ya kujua nani atapangwa kundi moja na nani.
Droo itafanyika Jumatano 19 Oktoba, 2016 saa mbili za jioni muda Afrika Mashariki.
FUFA watawakilishwa na Kamishna katika Wizara ya Elimu na Michezo Omara Apitta na kocha mkuu wa Uganda Cranes Milutin Sredejovic "Micho".

Mataifa yote 16 kila moja litatoa mwakilishi wake kufanya ziara kwenye miji minne vilipo viwanja, hoteli na viwanja vya mazoezi ambap fainali hizo zitafanyika AFCON 2017.
Uganda wamefuzu kushiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu 1978.

Vyungu AFCON 2017
Chungu 1: Gabon, Cote d’Ivoire, Ghana, Algeria
Chungu 2: Tunisia, Mali, Burkina Faso, DR Congo
Chungu 3: Cameroon, Senegal, Morocco, Egypt
Chungu 4: Togo, Uganda, Zimbabwe, Guinea Bissau

No comments: