Kizungumkuti cha suala la uongozi ndani ya chama cha wananchi CUF leo kimechukua sura mpya baada ya Baraza kuu la chama hicho kumvua uanachama aliyewahi kuwa mwenyekiti wake bara Bw.Ibahim Lipumba/
Katika kikao hicho kilichosimamiwa na Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmed Katani, wajumbe 43 waliohudhuria kati ya wajumbe 58,wamepitisha uamuzi wa kumvua uanachama Lipumba kwa tuhuma za kufanya vurugu,kuharibu mali za chama na kukataa wito wa chama.
Lipumba na wafuasi wake walihusika katika vurugu za mkutano wa chama hicho mwezi agosti, pia walivunja mageti na milango ya ofisi za chama cha CUF Dar es Salaam wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment