Kufikia sasa asilimia 42 ya kura za urais
nchini Kenya zimehesabiwa na kuwasilishwa rasmi kwa tume ya uchaguzi
IEBC kupitia mitambo ya electroniki.
Hata hivyo kumekuwepo malalamishi kuhusu kucheleweshwa kwa shughuli ya kujumlisha kura kutokana na hitilafu ya mitambo.
Uhuru Kenyatta, anayekabiliwa na
kesi katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, angali anashikilia
uongozi huku kura za urais zikiwa bado zinahesabiwa.Huu ni uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika tangu ghasia za baada ya mwaka 2007/2008 kufuatia matokeo yaliyozua utata.
Kenya iliendelea kuwa mbele kwa hesabu ya
matokeo ya mwanzo dhidi ya mpinzani wake waziri mkuu Raila Odinga katika
siku ya pili ya shughuli ya kuhesabu kura zaidi ya masaa 36 baada ya
shughili ya upigaji kura kukamilika.
Raila Odinga alidai kuibiwa ushindi wake mwaka
2007 wakati matokeo yalizua ghasia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya
laki moja huku maelfu wakiachwa bila makao.
Wakati mamilioni ya wakenya walijitokeza kupiga
kura kwa amani siku ya Jumatatu,watavyopokea matokeo ya mwisho ya kura
ndio itakuwa ishara ya uthabiti wa nchi hiyo.
Ni asilimia arobaini na moja ya kura zilizohesabiwa huku kukiwa na vituo zaidi ya elfu thelathini ambako kura zilipigiwa.
Ni zaidi ya kura milioni tano zilizohesabiwa kutoka kwa wapiga kura milioni 14.3 waliokuwa wamesajiliwa.
No comments:
Post a Comment