SOMALIA,
Mtu mmoja ameuawa na wengine kujeruhiwa katika
shambulizi la kujitoa mhanga nchini Somalia ambapo mshambuliaji
amejilipua karibu na ofisi za waziri mkuu
Mlinzi mmoja aliyeshuhudia shambulio hilo alisema kuwa polisi mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa.
Lakini kwa mujibu wa maafisa wa
utawala, watu wawili wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika
shambulio hilo lililotokea karibu na makao ya Rais mjni Mogadishu.
Mwandishi wa BBC Abdullahi Sheikh mjini Nairobi
anasema kuwa maafisa wakuu wanaelezea kuwa lengo la mshambuliaji
lilikuwa kulipua ofisi ya waziri mkuu Abdi Farah Shirdon.
Lakini wanajeshi waliokuwa wanashika doria walisema walimzuia kufika katika ofisi hiyo.
Aidha maafisa walidokeza kwamba mshambuliaji
alijilipua alipokuwa anahojiwa katika kizuizi kimoja cha polisi karibu
na ofisi hiyo.
Mshambuliaji alijilipua karibu na ukuta unaotenganisha ubalozi wa Ethiopia na makao ya waziri mkuu.
Majengo hayo mawili yako ndani ya eneo ambalo pia linahifadhi makaazi ya rais.
Idadi ya washambuliaji wa kujitoa mhanga imekuwa
ikipungua tangu wanamgambo wa Al Shabaab kuondoka Mogadishu kuanzia
Agosti 2011 lakini hili li dhihirsiho la changamoto inayowakabili
maafisa wa usalama katika kupambana na wanamgambo hao.(BBC)
No comments:
Post a Comment