DODOMA.
Polisi mkoani Dodoma imefanikiwa kumtia nguvuni Pascal Lawrent
Mkomoro 31 mkazi wa Mbabala B mjini hapa kwa tuhuma za mauaji ya
mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint John Lidya Leo Mzima aliyeuawa
kikatili usiku wa januari 20 mwaka huu, huku kukiripotiwa tukio jingine la uvamizi katika hosteli ya wanafunzi wa kike wa chuo hicho inayomilikiwa na mtu binafsi.
Marehemu Lidya ambaye alikuwa muuguzi wa hospitali ya Kilimatinde
iliyopo wilayani Manyoni Mkoani Singida anadaiwa kuuawa kinyama na watu
wasiojulikana kabla ya kutelekezwa porini na hatimaye kushambuliwa na
mnyama anayedhaniwa kuwa fisi.
Siku moja baada ya kuripotiwa kwa tukio la kuuawa kwa marehemu Lidya
Leo Mzima mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni Saint John,Jeshi la polisi
mkoani Dodoma lilitangaza msako mkali mjini hapa
ambapo harakati hizo Bi.Getrude Mamboleo 34 mkazi wa Mbabala B
alikutwa na simu ya mkononi inayodaiwa kuwa mali ya marehemu na baada ya
kubanwa na askari alimtaja mtuhumiwa kuwa ndiye aliyemuuzia kwa thamani
ya shilingi 20,000.
Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP David Misime alithibitisha kuwa
Mtuhumiwa Lawrent au maarufu kwa jina la Bopa anadaiwa kukiri kuhusika
na tukio hilo kwa asilimia mia moja huku akiweka bayana kushiriki
matukio mbalimbali ya kihalifu.
Kifo cha marehemu Lidya aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 57
kimeacha simanzi kwa maelfu ya wakazi wa mkoa wa Dodoma hususani
wanafunzi wa chuo cha Saint John ambao wamebaki na hofu ya usalama wa maisha yao
kutokana na chuo hicho kuandamwa na matukio ya kutisha mara kadhaa.
Wakati juhudi za kuwasaka watuhumiwa wengine wa mauaji hayo zikipamba
moto, mwili wa Marehemu Lidya umezikwa jumanne hii katika kijiji cha
Matombo mkoani Morogoro.
Wakati huo huo: Kumeripotiwa tukio la wanafunzi wengine katika hosteli ya wanafunzi wa kike inayomilikiwa na mtu binafsi kuvamiwa kuporwa na kunusurika kubakwa usiku wa kuamkia leo, taarifa za awali zimeeleza kuwa majambazi hao waliwavamia wanafunzi usiku wa kuamkia leo, hali iliyosababisha
Thursday, January 24, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment