DAR ES SALAAM-TANZANIA,
TIMU ya Yanga leo imeichapa Mgambo JKT ya Handeni, Tanga mabao 3-0
kwenye mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Ushindi huu, unaifanya Yanga iwe na pointi sawa na mabingwa watetezi,
Simba SC waliotoka sare ya 1-1 na Polisi Morogoro uwanja wa Jamhuri
Mpaka timu zinakwenda mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0,
yaliyofungwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Didier
Kavumbangu.
Cannavaro alifunga kwa kichwa krosi ya Oscar Joshua dakika ya pili,
wakati Kavumbangu alimalizia pasi ya Hamisi Kiiza dakika ya 39.
Kipindi cha pili, Yanga walirudi na moto wao tena na kuendelea
kuliandama lango la Mgambo JKT na Yanga dakika 34 kupata bao la tatu,
mfungaji akiwa ni Jerry Tegete aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi
ya Kavumbangu.
Mgambo JKT ilipata pigo dakika ya 85, baada ya beki wake wa kulia, Salum
Mlima kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu
mbaya Mbuyu Twite.
Kikosi cha Yanga; Ally Mustafa ‘Barthez’, Nsajigwa Shadrack, Oscar
Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’,
Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Hamisi Kiiza na Haruna
Niyonzima.
Mgambo JKT; Godson Mmasa, Salum Mlima, Yassin Awadh, Salum Kipanga,
Bakari Mtama, Ramadhani Malima, Chande Magoja, Mussa Ngunda, Issa
Kandulu, Fully Maganga na Juma Mwinyimvua
Katika mchezo wa Simba uliochezwa mjini Moro kwenye uwanja wa Jamhuri
ilitoka sare ya 1-1 na Polisi na wenyeji wakitangulia kupata bao dakika
ya 35 kupitia kwa Mokili Rambo na Amri Kiemba alisawazisha dakika ya 57.
Thursday, November 1, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment