TRENI YAGONGANA NA BASI MISRI NA KUUA WATOTO 50-WAZIRI WA USAFIRI AJIUZULU - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Sunday, November 18, 2012

TRENI YAGONGANA NA BASI MISRI NA KUUA WATOTO 50-WAZIRI WA USAFIRI AJIUZULU

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02401/Egypt-train-crash_2401756c.jpgCAIRO-MISRI,         Ajali hiyo imetokea leo saa mbili asubuhi kwa saa za huko katika jimbo la Asyutu kusini mwa Misri. Gavana wa jimbo hilo Yahya Kishkik pamoja na maofisa kadhaa wamekwenda kwenye eneo la ajali na kutaka kuunda haraka kamati ya uchunguzi. Pia ametoa salamu za rambirambi kwa familia za watu walioathirika huku akisihi itolewe fidia kwa watu waliofariki na kujeruhiwa.
Treni moja nchini Misri imegongana na basi la shule na kusababisha vifo vya watoto 50.

Wakati huohuo Habari zaidi zinasema kutokana na ajali hiyo, waziri wa usafiri nchini humo Mohamed Rashid el-Matin amejiuzulu kuonesha uwajibikaji baada ya ajali hiyo ambayo serikali ndiyo inalaumiwa kutokana na kuwa na miundo mbinu mibovu ikikumbukwa ajali kubwa ya treni mwaka 2002 ambapo watu 360 walikufa  baada ya treni kuwaka moto.

 Rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi amemtaka waziri mkuu Hesham Gandil kutoa msaada wowote wa lazima utakaohitajika na kuwatibu waliojeruhiwa na kuahidi kuwaadhibu wale wote waliosababisha ajali hiyo.

No comments: