AFRIKA KUSINI KUCHAPISHA NOTI ZENYE PICHA YA MANDELA - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Thursday, November 1, 2012

AFRIKA KUSINI KUCHAPISHA NOTI ZENYE PICHA YA MANDELA


JOHANESBURG-AFRIKA KUSINI,
Afrika Kusini inatarajia kuchapisha noti mpya zenye picha ya rais Mandela mapema mwezi huu, kuonyesha heshima yao kwa rais huyu wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.

Gavana wa Benki Kuu ya Afrika Kusini Gill Marcus amesema,noti hizo mpya zitatumika rasmi kuanzia tarehe 6 ya mwezi huu. Upande mmoja wa noti hizo utakuwa na picha ya rais wa zamani Mandela, na upande mwingine utakuwa na picha za wanyamapori maarufu watano wenye sifa barani Afrika. Gavana huyo amesema noti hizo mpya ni za Rand 10, 20, 50, 100 na 200, na zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia mpya itakayosaidia kugundua noti bandia.

Ili kuwafahamisha wananchi noti hizo, serikali ya Afrika Kusini imefanya shughuli husika za matangazo nchini humo pamoja na nchi za kanda hiyo ambako fedha ya Afrika Kusini inatumika zikiwemo Namibia, Swaziland, na Lesotho.(Chanzo:Idhaa ya China)

No comments: