UINEREZA VS UFARANSA HAKUNA MBABE. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Tuesday, June 12, 2012

UINEREZA VS UFARANSA HAKUNA MBABE.

UKRAINE,Ufaransa walijitutumua kutoka nyuma na kulazimisha sare ya goli 1-1 dhidi ya Uingereza hapo jana katika mechi ya ufunguzi wa mechi za kundi D.

Mlinzi wa Manchester City Joleon Lescott aliipatia Uingereza goli la kuongoza katika dakika ya 30 baaada ya kupata krosi safi kutoka kwa Stephen Gerard.

Dakika tisa baadaye Samir Nasri Aliisawazishia timu yake baada ya kupiga shuti la chini nje ya eneo na kuipa mgawanyo wa pointi timu yake.

Katika mchezo huo timu hizo ziligawana utawala ambapo kipindi cha kwanza kilitawaliwa na Ufaransa na kile cha pili kiltawaliwa na Uingereza.
Leo tena michuano hiyo inaendelea ambapo kutakuwepo mechi za kundi A zitakazozikutanisha timu za Ugiriki dhidiya Jamhuri ya Czech na Poland watakaovaana na Urusi.

Greece v Czech Republic
Poland v Russia

No comments: