SUDAN YA KUSINI YAPOKWA DOLA BILIONI 4-Rais Kiir azitaka zirudishwe. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Wednesday, June 6, 2012

SUDAN YA KUSINI YAPOKWA DOLA BILIONI 4-Rais Kiir azitaka zirudishwe.











sudan kusini
http://www.mideastnewswire.com/wp-content/uploads/2011/02/Salva_Kiir_Khartoum.jpg
Rais Salva Kiir
 Zaidi ya dola bilioni 4 (sawa na zaidi ya Trilioni 6 za kitanzania) Zimeibiwa kutoka Serikali ya Sudan ya Kusini kutokana na ufisadi imebainika. Ufisadi huo umewahusisha viongozi 75 wa ngazi ya juu wakiwemo mawaziri na viongozi wengine wa serikali. Fedha hizo ni pamoja na zaidi yadola bilioni 2 zilizopotea kutokana na ufisadi katika mauzo ya zao la mtama na nyingine katika mafuta.
Rais wa Sudan Bw. Salva Kiir amewaandikia barua wakuu hao akiwataka kuzirudisha fedha hizo ama sivyo watakutana na mkono mkali wa sheria.Kupitia barua alizowaandikia wakuu hao Rais huyo ameonekana kuudhika sana na kitendo hicho akiwaambia wakuu hao waliweka maslahi ya o mbele zaidi ya taifa'
"Raia wa Sudan Kusini wanapata taabu lakini viongozi hawa wanafikiria tu tamaa zao binafsi" alisema Rais Kiir katika barua hiyo.
Rais Kiir amesema sehemu kubwa ya fedha hizo imewekwa kwenye akaunti zilizo nchi za kigeni  na nyingine kununua mali au majengo katika nchi hizo.

Sudan ya Kusini ambayo ilijitenga naSudan Kaskazini nakuwa taifa huru mnamo mwezi Julai mwaka Jana inategemea mafuta kwa asilimia 98 ya kipato chake ambapo kwa sasa imesimamisha uzalishaji wa mafuta hayo kutokana na mgogorio wake na Sudanya Kaskazini nahivyo kuwa na hali ngumu katika kutoa huduma za kijamii.

No comments: