DAR ES SALAAM, TANZANIA.
Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Dr.Arison Mwakyembe aetengua uteuzi wa Kaimu mkurugenzi wa Shirika la ndege la Tanzania(ATCL) bw Paul Chizi na kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne kwa kukiuka sheria taratibu na kanuni za utumishi wa umma.
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa wizara hiyo Bw.Omary Chambo kwawaandishi wa habari, Waziri huyo amefikia uamuzi huo kutokana nauteuzi wa Kaimu mkurugenzi huyo kutofuata utaratibu, “Uteuzi wake haukufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, hivyo kupitia Sheria Na 8 ya mwaka 2002 na kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2003 Na 17(4), Dk Mwakyembe ametengua uteuzi huo kuanzia jana.” alisema katibu Mkuu huyo.
Kutokana na utenguzi huo Waziri mwakyembe amemteua Kapteni Lusajo Lazaro kuwa kukaimu nafasi hiyo.
Waziri huyo pia amewasimamisha wakurugenzi wengine wanne ambao ni Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara, Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi, John Ringo, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Josephat Kagirwana Mwanasheria wa ATCL, Amini Mziray. .
Kwa mujibu wa katibuhuyo pia itaundwa tume maalum kuchunguza matumizi ya fedha kuanzia mwezi Mei mwaka huu.
Wednesday, June 6, 2012
New
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment