LOWASSA AWASHUKIA MAADUI WAKE. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Monday, June 4, 2012

LOWASSA AWASHUKIA MAADUI WAKE.

ARUSHA, TANZANIA

Waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa  amewashukia maadui zake anaodai wanamchafua kisiasa na kuwaambia kuwa hawamnyimi usingizi na yeye anamtumainia Mungu.

Lowassa aeyasema hayo katika harambee ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) usharika wa Elaira mkoani Arusha ambapo alikuwa moja ya wageni waalikwa.
Bila kuwataja maadui hao Lowassa alisema kuna baadhi ya watu wantumia vyombo vya habari kumchafua kisiasa lakini hawamnyimi usingizi.

“Nakushukuru Baba Askofu kwa kunijibia, wale wote wanaonisemasema kwenye magazeti wala hawanisumbui na wala hawaninyimi usingizi,” alisema Lowasa akiunga mkono kauli ya Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer aliyemtaka kuendelea kufanya kazi ya Mungu licha ya baadhi ya watu kumkatisha tamaa.iongezaAlisema anamtumainia Mungu na wala hawaogopi maadui zake.

No comments: