CUF WAJUNGA KUPINGA BAJETI - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Sunday, June 17, 2012

CUF WAJUNGA KUPINGA BAJETI






https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZH5Zc3m379VNLVfGlAYOAHLVcat60IOANYDq3W6yY6ASyWb3zya64t0KtyF2AXbLWN5ZsW1qmUZ_6-YKGA22RQEhsFraCdnfQ6o6XqgsEMwgtmSCWUlMW_wY0WGbwW93RFNrxwpF_exgs/s400/lipumba.jpg






 DODOMA,
 Chama cha wananchi CUF kupitia kwa mwenyekiti wake Prof. Ibrahim Lipumba kimeungana na  vyama vingine vya siasa vya upinzani kupinga Bajeti ya Serikali ya 2012/2013.

Lipumba aliiponda Serikali akisema kuwa nchi inahitaji uongozi wenye uwezo wa kusimamia rasilimali za nchi na matumizi ya fedha za umma.

Akiongea kwa niaba ya chama chake  mwenyekiti huyo amesema katu chama chake hakitaiunga mkono bajeti hiyo kwani  serikali imeshindwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na pia imekuwa na usimamizi mbovu wa vyanzo vilivyopo.

Kwa tamko hilo , Lipumba ameungana na wenyeviti wenzake wa vyama vya upinzani, Freeman Mbowe wa Chadema na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi ambao kwa wakati tofauti walisema bajeti hiyo haina jipya na imelenga kuwanufaisha watu wachache.

No comments: