MAGAIDI WASHAMBULIA HOTELI KENYA. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Wednesday, May 16, 2012

MAGAIDI WASHAMBULIA HOTELI KENYA.

Polisi akilinda eneo la tukio usiku huu.

Magaidi wameshambulia hoteli maarufu ya Bella Vista Restaurant,iliyopo pembezoni mwa bara bara ya kwenda Mombasa na kuua mtu mmoja huku wakijeruhi wengine watano.
Polisi wanasema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na milipuko mitatu katika klabu hiyo ya Bella Vista Restaurant ambayo ni kutoka katika guruneti zilizorushwa kuelekea hotelini hapo.
Milipuko hiyo ilisababisha uharibifu wa magari sita yaliokuwa yameegeshwa kando ya hoteli hiyo.
Mkuu huyo wa polisi alisema wanaamini shambulio hilo lilitekelezwa na magaidi.

Inadaiwa kuwa watu wawili walikwenda katika Klabu hicho wakitaka kuruhusiwa kuingia.
Lakini walipotakiwa kukaguliwa  na maaskari wa hoteli hiyo walikataa na ndipo wakarusha maguruneti hayo.
 Mmoja wa watu waliokuwa karibu na eneo hilo ameiambia AFP kuwa aliwaona watu wakikimbia baada ya mlipuko mkubwa.
mashuhuda wa tukio wamedai watu hao walifyatua risasi hovyo wakati wakiondoka huku polisi wakisema bado hawajamkamata mtu yeyote kuhusianan na tukio hilo.

Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya milipuko ambayo yamelenge vituo vya polisi, |Makanisa na baa za pombe hivi karibuni baada ya kenya kuivamia Somalia na kupambana na wanamgambo wa Alshabab, na pengine tukio hili litahusishwa na kikundi hicho


No comments: