MAELFU WAKIMBIA MAPIGANO DRC - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Saturday, May 19, 2012

MAELFU WAKIMBIA MAPIGANO DRC

Moja ya kundi la wakimbizi wakiwa njiani Goma.

Bunagana, DR Congo - Mapigano yanayoendelea huku Kivu Kaskazini mashariki ya Kongo yamewalazimisha wakazi wa maeneo hayo kukimbilia nchi za jirani za Rwanda na Uganda kuokoa maisha yao.Wanawake na watoto ni moja ya kundi kubwa katika msafara huo.


Wananchi hao wanakimbia kuhofia kushambuliwa na waasi wanaoipinga  serikali ya kinshasa wakiongozwa naaliyekuwa kamanda wa jeshi la kongo Jenerali Ntaganda.
Tumesikia mapigano kati ya waasi na Serikali, kwa hiyo tumekimbia huku kujiokoa kwa sababu kubaki kule ni kuhatarisha maisha yetu" alisema kajambere seberera  ambaye yupo nchini Uganda baada ya kukimbia mapigano hayo.


Hata  hivyo hali sio nzuri katika kambi za UNHCR  Kisoro nchini Uganda ambapo licha ya kufunguliwa sehemu hiyo bado chakula, malazi na maji vimekuwa ni tatizo.Baadhi ya wakimbizi hao wamelazimika kulala nje huku wengine wakirudi Kongo mchana kutafuta maji na Chakula.


Hali imekuwa ngumu zaidi kwa watoto na akinamama waliovuka mipaka ambao idadi yao ni kubwa.


Mapigano hayo kati ya majeshi ya serikali na yale ya majeshi ya Kamanda muasi Jenerali Ntaganda yalianzayamesababisha usumbufu mkubwa katika eneo hilo la Kivu na maeneo menginene nchini humo.

No comments: