UCHAGUZI SENEGAL KUINGIA DURU YA PILI - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Monday, April 23, 2012

UCHAGUZI SENEGAL KUINGIA DURU YA PILI



DAKAR, SENEGAL,
                               Ikiwa Zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa kugombea urais Jumapili iliyopita nchini Senegal zimekwishakuhesabiwa, matokeo yanaonesha dhahiri uwezekano wa kuwepo Duru ya pili ya Uchaguzi huo baada ya mshindi wa moja kwa moja kushindwa kupatikana hadi hivi sasa. Matokeo hayo yanaonesha rais wa aliyepo madarakani Bw.Abdoulaye Wade akiongoza kwa asilimia 32.17 huku mpinzani wake wa karibu na waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Bw.Macky Sall akimfuatia kwa kura 25.24, ilhali mshindi akihitajika kuwa na asilimia 50 au zaidi ya kura zote.

Rais Wade ambaye alijitapa kuibuka mshindi siku ya jumapili alipomaliza kupiga kura, amekiri kuwa mambo ni magumu na kusema yote yanawezekana ya pengine yeye kushinda moja kwa moja  au kuingia duru ya Pili na mpinzani wake mkuu Bw. Sall, Huku msemaji wake hapo jana  akikiri  kuwa kweli hali ipo wazi kuwa uchaguzi huo utaingia duru ya pili. Matokeo toka wilaya 282 kati ya jumla ya wilaya 551 yamekwishahesabiwa na yanaendelea kutangazwa katika vyombo mbali mbali vya habari nchini humo huku tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ikisubiri kuyatangaza rasmi siku ya Ijumaa hii.

Ikiwa uchaguzi huo utaingia duru ya pili hiyo itakuwa ni habari mbaya kwa Rais Wade ambaye sasa atakwenda kupambana na wapinzani waliounganisha nguvu zao kumuunga mkono mpinzani mwenzao Bw. Sall.
 Senegal ambayo inaaminiwa kuwa nimoja ya nchi zenye demokrasia barani Afrika imeingia dosari hivi karibuni baada ya rais wa nchi hiyo aliyepo madarakani Bw.Abdoulaye Wade kung'ang'ania kugombea katika awamu ya tatu baada ya kumaliza vipindi vyake viwili vya uongozina kusababisha  vurugu pamoja na maandamano yaliyoshuhudia matumizi ya nguvu kutoka kwa vikosi vya Usalama hali inayolaaniwa na Wanaharakati na Wapinzani nchini humo.
Hata hivyo ucrudiaji wa uchaguzi huo ni suala la kusubiri kwani kwa sasa lolote laweza kutokea na pengine mshindi wa moja kwa moja akapatikana.














No comments: