JUBA/ADDIS ABABA, Sudan ya kusini leo imefunga rasmi usafirishaji wa mafuta yake kuelekea Sudani ya Kaskazini hadi pale matakwa yake yatakapotekelezwa.matakwa yanayohusiana na kulipwa deni lake la dola bilioni 2.4, kuacha kuwasaidia waasi na kuachia eneo linalogembewa na mataifa hayo mawili la Abyei pamoja na kuchorwa kwa mpaka kamili wanchi hizo mbili.
Akiongea kwa niaba ya Serikali yake waziri wa mafuta wa Sudan ya Kusini Bw.Stephen Dhieu Dau amesema Sudan ya kusini imesimamisha usafirishaji wa mapipa yapatayo 350,000 kwa siku kwenda Sudan kaskazini " ufungaji huo ni asilimia 100 na usafirishaji wake utaanza mpaka pale makubaliano yatakapofikiwa na kusainiwa' alisema waziri huyo.Waziri huyo alisema Sudan ya kaskazini ni lazima iheshimu mipaka iliyaokubaliwa mwaka 1956 na hivyo kurudisha maeneo yote iliyoyapora kutoka kwa Sudan ya Kusini.
Akiongea katika baraza la umoja wa Afrika katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa bw. Ban ki moon alisema ana wasi wasi kuwa mgogoro huo utapelekea matumizi ya silaha na kuleta vita na akawalaumu marais wa nchi hizo mbili kwa kushindwa kufikia makubaliano.
Sudan ya kaskazini ambayo imepata uhuru wake mwaka jana mwezi julai inaituhumu Sudan ya kusini kwa Kuipokonya eneo la abyei ambalo lina utajiri wa mafuta kwa kuweka vikosi vyake tangu mwaka jana, pia kwa kukisaidia kikundi cha Sudan People's Liberation Movement North (SPLM-N) kinachoipinga serikali ya Sudan Kusini pia inalalamikia gharama za usafirishaji mafuta inazotozwa na Sudan ya Kaskazini ambayo ndio mmiliki wa mabomba yanayosafirisha mafuta hayo licha ya Sudan ya Kaskazini kumiliki robo tatu ya eneo hilo. marais wa nchi hizo walikutana ijumaa iliyopita na kushindwa kufikia makubaliano.
Sunday, April 22, 2012
New
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment