Rais wa Benin Thomas Boni Yayi, achaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Sunday, April 22, 2012

Rais wa Benin Thomas Boni Yayi, achaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika.

  Adis Ababa,Ethiopia,

  Viongozi kutoka nchi 54 za afria wamemchagua rais wa benin Bw. Thomas                                               Boni Yayi kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja huo akimbadili rais wa  Guinnea ya Ikweta bw. Teodoro Obiang Nguema aliyetumikia kwa mwaka mmoja uliopita. Akipokea wadhifa huo Rais huyo ameelezeaa furaha yake yakupewa heshima hiyo na kuahidi Kudumisha amani barani Afrika.


   Baraza hilo la umoja wa Afrika Linalokutana  kwa muda wa siku mbili mjini Adis Ababa kesho linatarjiwa kumchagua mkuu wa baraza la usalama na Amani ambaye pia atakuwa anampokea wadhifa huo ndugu
Jean Ping kutoka Gabon aliyekuwa madarakani tangu mwaka 2008, anayegombea nafasi hiyo ni mke wa zamani wa rais wa sasa Afrika kusini Bw.Jacob Zuma mama  Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani ya Afrika kusini.Afrika kusini imesema inaimani mama huyo atshinda na kuchukua wadhifa huo kutoka kwa Bw. jean Ping.

                                                                                                                                                                     Katika mkutano huo wa 18 wa kilele ajenda muhimu zinazojadiliwa ni pamoja na kuimarishwa bishara Afrika, mzozo wa Somalia, mgogoro wa mafuta kati ya Sudan na Suda kusini na pia suala la viongozi wa Afrika kung'ang'ania madaraka.  




No comments: